Habarika | KAMPUNI ZA SIMU ZINAZOTOA HUDUMA YA FEDHA ZAENDELEA KUNEEMEKA: ZAVUNA TRILIONI 13 MIEZI MIWILI ILIYOPITA
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

KAMPUNI ZA SIMU ZINAZOTOA HUDUMA YA FEDHA ZAENDELEA KUNEEMEKA: ZAVUNA TRILIONI 13 MIEZI MIWILI ILIYOPITA

Kampuni za simu zinazotoa huduma ya fedha kwa njia ya simu za mkononi katika kipindi cha miezi miwili iliyopita Novemba na Desemba mwaka jana zimekusanya kiasi cha Sh. trilioni 13.07.
Kaimu Meneja wa Habari Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala amesema kuna ongezeko kubwa la matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya mtandao hapa nchini.

Amesema kuwa katika miezi miwili iliyopita mwaka jana ambapo Novemba walikusanya Sh.trilioni 6.47 na Desemba Sh.trilioni 6.60 jumla ya makusanyo yote ni sh. Trilioni 13.07 kuptia kampuni za simu zinazohusika na huduma ya miamala.

Alitaja kampuni zilizohusika na maiamala hiyo ni pamoja na Zantel(Easy Pesa),Tigo (Tigo pesa), Vodacom(Mpesa), Aiterl(Airtel Money na Halotel (Halopesa).

Aidha aliwataka wananchi kujihadhari na utapeli unaofanywa kwa kutumia simu za mkononi huku mamlaka na vyombo vya usalama vinashughulikia suala hilo.

 

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By