Habarika | JESHI LA POLISI LAAGIZWA KUFANYA UCHUNGUZI JUU YA UPORWAJI BUNDUKI KWA ASKARI
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

JESHI LA POLISI LAAGIZWA KUFANYA UCHUNGUZI JUU YA UPORWAJI BUNDUKI KWA ASKARI

Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amelitaka jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio la askari kuporwa bunduki aina ya SMG na kisha kuwachukulia hatua za kinidhamu askari watakaobainika kuzembea katika tukio hilo.

Rugimbana ametoa kauli hiyo ikiwa ni wiki moja tangu askari polisi PC Shadrack kuporwa bunduki na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Ofisa Mawasiliano ya serikali Mkoa wa Dodoma, Jeremiah Mwankyoma alisema mkuu wa mkoa ameliagiza jeshi jilo kujipanga vizuri kuhakikisha tukio hilo linakuwa la mwisho na halitokei tena

“Mkuu wa mkoa ameliagiza jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo kubaini kama kuna dalili zozote za kuwapo kwa uzembe na endapo itabainika kulikuwa na uzembe Jeshi la Polisi lichukue hatua kali kwa askari waliohusika”, alisema

Pia aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuwabaini wahusika ili kukomesha matukio kama hayo

Alhamisi iliyopita askari huyo aliporwa silaha hiyo na watu saba wanaosadikika kuwa majambazi katika Ofisi ya Kampuni ya Simu ya Halotel iliyopo Medelii, Kata ya Makole, Manispaa ya Dodoma

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By