Habarika | JESHI LA KENYA LAUA WANAMGAMBO 21 WA AL SHABAB
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

JESHI LA KENYA LAUA WANAMGAMBO 21 WA AL SHABAB

Jeshi la Kenya linasema kuwa limewaua wapiganaji 21 wa kundi la al-Shabab nchini Somalia.

Jeshi liliwawinda wanamgambo hao baada ya msafara wao kushambuliwa magharibi mwa Somalia, kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo.

Al-Shabab inasema kuwa wapiganaji wake waliwaua wanajeshi watano , wakawajeruhi wanne na kuchoma gari moja la kijeshi wakati wa mapigano hayo ambapo Jeshi la kenya halikusema ikiwa lilikumbwa na maafa yoyote.

Wanajeshi wa Kenya waliingia nchini Somalia mwaka 2011, kuwapiga vita wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.

-BBC Swahili

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By