Habarika | JAPAN YAADHIMISHA MIAKA MITANO YA TSUNAMI
layout-wrap boxed
Saturday, March 24, 2018

JAPAN YAADHIMISHA MIAKA MITANO YA TSUNAMI

Taifa la Japan linaadhimisha miaka mitano tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi na Tsunami iliosababisha vifo vya watu 18,000 wengine wakiwa hawajulikani waliko.

Waziri mkuu Shinzo Abe na mfalme Akihito wamehudhuria makumbusho ya janga hilo mjini Tokyo na walikaa kimya kwa muda ili kutoa heshima kwa wale walioathiriwa.

japa

Ukubwa wa tetemeko hilo la 9.0 katika vipimo vya richa lilipiga ufukwe wa bahari wa taifa hilo na kusababisha maji kujaa hatua iliyosababisha uharibifu mkubwa kaskazini mashariki mwa pwani ya taifa hilo.

Pia mafuriko hayo yalisababisha janga baya la kinyuklia katika kinu cha fukushima Daiichi baada ya maji kuingia katika kinu hicho na kuathiri mashine za baridi hatua iliyosababisha mmomonyoko.

-BBC SWAHILI

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By