Habarika | ICC YASITISHA KESI ILIYOKUWA IKIMKABILI WILLIAM RUTO
layout-wrap boxed
Tuesday, December 12, 2017

ICC YASITISHA KESI ILIYOKUWA IKIMKABILI WILLIAM RUTO

ruto

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) imeamua kuwa Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto hana kesi ya kujibu kuhusiana na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yanamkabili.

Aidha, imeamua pia kwamba mwanahabari Joshua arap Sang, aliyeshtakiwa pamoja na Bw Ruto, hana kesi ya kujibu.

Bw Ruto alikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya watu takribani 1,200, kuhamisha watu kwa lazima na mateso yaliyotekelezwa wakati wa vita vya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo alikana mashtaka hayo na mawakili wake walitaka kesi hiyo itupiliwe mbali kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Majaji wamesema upande wa mashtaka haukutoa ushahidi wa kutosha kuthibitisha madai dhidi ya Bw Ruto na Bw Sang.

Desemba mwaka 2014, mwendesha mashtaka aliondoa mashtaka sawa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta akisema mashahidi walikuwa wametishiwa na kubadilisha ushahidi wao.

Bw Ruto na Bw Kenyatta walikuwa kwenye kambi pinzani wakati wa uchaguzi wa 2007 lakini waliunda muungano wa kisiasa na wakashinda uchaguzi mkuu wa 2013.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/icc-yasitisha-kesi-iliyokuwa-ikimkabili-william-ruto/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By