Habarika | HOFU YATANDA ARUSHA, SHEHENA YA VYAKULA NA VIPODOZI VILIVYOISHA MUDA YAKAMATWA
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

HOFU YATANDA ARUSHA, SHEHENA YA VYAKULA NA VIPODOZI VILIVYOISHA MUDA YAKAMATWA

Maafisa kutoka Mamlaka ya chakula na dawa Kanda ya Kaskazini wamefanya operesheni ya ghafla kwenye maduka makubwa ya chakula na kukamata shehena ya vyakula, maziwa na vipodozi vilivyoisha muda wa matumizi huku baadhi ya wauzaji wakikimbia kuogopa wakaguzi.

katika operesheni hiyo iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha wakaguzi wamefanikiwa kukamata idadi kubwa ya vyakula maziwa na vipodozi vilivyo isha muda wa matumizi huku baadhi ya wauzaji wakionekana kukimbia wakaguzi
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha ambao ndiyo watumiaji wa bidhaa hizo wamesema wamepatwa na mashaka makubwa kupatwa na magonjwa kama kansa na mengine na kuiomba Serikali ichukue hatua kali kwa wahusika wanaocheza na afya za binadamu huku mkaguzi mwandamizi wa TFDA Abdallah Mkanza akidai zoezi ilo ni endelevu.
Kifungu cha 6(c) namba 34,35,na 99 cha sheria ya chakula dawa na vipodozi kimeipa TFDA mamlaka ya kuzuia na kuharibu bidhaa zisizo na kiwango kinacho takiwa kwa matumizi ya binadamu.
Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By