Habarika | HIZI NDIZO KAULI SITA ZA MAKONDA ZILIZOMPONZA WILSON KABWE KWA MAGUFULI
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

HIZI NDIZO KAULI SITA ZA MAKONDA ZILIZOMPONZA WILSON KABWE KWA MAGUFULI

“Mkataba moja ulisainiwa Januari 30, mwaka jana kwa kutumia sheria ndogo ya mwaka 2009 na mwingine ulisainiwa Januari 31, mwaka huu kwa kutumia mkataba wa mwaka 2004 na mbaya zaidi mikataba yote hii imesainiwa na mtu mmoja Kabwe,”

“Lakini cha kushangaza tumebaini kuwa bado kampuni inayokusanya mapato katika kituo cha Ubungo, inawasilisha mapato hayo kwa kutumia sheria ya mwaka 2004 yaani Sh milioni 42 badala ya Sh milioni 82 kwa mwezi…” …” Mbaya zaidi kamati ile katika ukaguzi wake, ilikuta kampuni ya ukusanyaji mapato hayo stendi ya Ubungo inayo Sheria ya mwaka 2009 lakini katika nyaraka za Halmashauri ya Jiji zinaonyesha sheria inayotumika ni ya mwaka 2004,”

“Ukipiga hesabu za harakaharaka utagundua kuwa kila mwezi Sh milioni 42 zimekuwa zikipotelea kwenye mikono ya wachache, kwa maana hiyo kuanzia mwaka 2009 Sh bilioni tatu zimepotea na kila mwaka tumekuwa tukipoteza Sh milioni 500, huu ni ufisadi wa aina yake kwa kweli,”

“Kwa mujibu wa taratibu, kila kibanda mle ndani ya stendi kinatakiwa kukodishwa kwa Sh 100,000 hadi Sh 200,000 kwa mwezi, lakini tumebaini kuwa wapo watu wachache wamevihodhi na kuvikodisha kwa zaidi ya Sh milioni 1.5, kwa mwezi,”

“Kiutaratibu mheshimiwa Rais, mkataba unapoisha lazima ufanyike mchakato wa kutafuta mzabuni mpya na hata mwekezaji aliyepo anaruhusiwa kushiriki kuomba tena, lakini kilichofanyika ni kinyume kabisa, wakati tunajua kwa sasa eneo la mapato ya maegesho ni kubwa na maeneo mengi yameongezeka kuna nini hapa?

“Naomba Takukuru waendelee na uchunguzi wa suala hili ili waliohusika na haya wachukuliwe hatua,”

 

RAIS John Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe kutokana na kashfa ya ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya stendi ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya mji.

Hatua hiyo ya Rais Magufuli, imetokana na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuwasilisha mbele yake taarifa ya Kamati aliyoiteua kwa ajili ya kuchunguza kwa undani utekelezwaji wa mikataba hiyo hasa katika eneo la mapato.

Makonda aliwasilisha ripoti hiyo Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa daraja jipya na la kisasa kuliko yote Afrika Mashariki na Kati la Kigamboni, ambalo kwa sasa limepewa jina jipya na Rais Magufuli la Daraja la Nyerere.

 

Awali akitambulisha viongozi wa mkoa waliohudhuria sherehe za uzinduzi huo, RC Makonda, pamoja na mambo mengine alibainisha kuwa muda mfupi tangu ashike wadhifa wa Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliunda kamati ndogo kwa ajili ya kuchunguza mikataba katika stendi ya Ubungo na wa maegesho ya magari katikati ya jiji.

Alisema kamati hiyo ilibainisha mambo mengi yanayofedhehesha kuhusu mikataba hiyo, likiwemo suala la Mkurugenzi wa Jiji Kabwe, kusaini mikataba miwili tofauti ya ukusanyaji wa mapato katika stendi hiyo ya Ubungo kwa kutumia sheria ndogo tofauti ikiwemo iliyopitwa na wakati.

“Mkataba moja ulisainiwa Januari 30, mwaka jana kwa kutumia sheria ndogo ya mwaka 2009 na mwingine ulisainiwa Januari 31, mwaka huu kwa kutumia mkataba wa mwaka 2004 na mbaya zaidi mikataba yote hii imesainiwa na mtu mmoja Kabwe,” alisema Makonda.

Alifafanua kuwa Sheria ndogo ya mwaka 2004 ya ukusanyaji mapato ndani ya kituo hicho, inaonesha kuwa kila basi linatakiwa kutozwa Sh 4,000 hivyo makusanyo halisi kwa mwezi ni Sh milioni 42 kutokana na mabasi 350 yanayoegeshwa kituoni hapo.

Hata hivyo, alisema kutokana na mabadiliko ya tozo, sheria hiyo ilibadilishwa mwaka 2009 na kila basi likawa linatozwa Sh 8,000 na hivyo makusanyo ya mwezi yakapanda na kufikia Sh milioni 82 kwa mwezi.

“Lakini cha kushangaza tumebaini kuwa bado kampuni inayokusanya mapato katika kituo cha Ubungo, inawasilisha mapato hayo kwa kutumia sheria ya mwaka 2004 yaani Sh milioni 42 badala ya Sh milioni 82 kwa mwezi…” …” Mbaya zaidi kamati ile katika ukaguzi wake, ilikuta kampuni ya ukusanyaji mapato hayo stendi ya Ubungo inayo Sheria ya mwaka 2009 lakini katika nyaraka za Halmashauri ya Jiji zinaonyesha sheria inayotumika ni ya mwaka 2004,” alisisitiza Makonda.

Kwa mujibu wa Makonda, kwa hali ilivyo tangu sheria ndogo ya mwaka 2009 ipitishwe haijawahi kutumika na hivyo kulisababishia hasara jiji hilo ya Sh bilioni tatu kutokana na mapato katika stendi hiyo kuendelea kuwasilishwa kwa kutumia sheria ya mwaka 2004.

“Ukipiga hesabu za harakaharaka utagundua kuwa kila mwezi Sh milioni 42 zimekuwa zikipotelea kwenye mikono ya wachache, kwa maana hiyo kuanzia mwaka 2009 Sh bilioni tatu zimepotea na kila mwaka tumekuwa tukipoteza Sh milioni 500, huu ni ufisadi wa aina yake kwa kweli,” alisema.

Aidha Makonda alisema pia kamati yake iligundua aina nyingine ya ufisadi ndani ya kituo hicho cha Ubungo kwa baadhi ya watu wakiwemo vigogo kuhodhi mabanda ya biashara yaliyomo ndani ya kituo hicho na kutoza kodi kubwa zaidi ya mara 10 ya ile inayostahili.

“Kwa mujibu wa taratibu, kila kibanda mle ndani ya stendi kinatakiwa kukodishwa kwa Sh 100,000 hadi Sh 200,000 kwa mwezi, lakini tumebaini kuwa wapo watu wachache wamevihodhi na kuvikodisha kwa zaidi ya Sh milioni 1.5, kwa mwezi,” alisema.

Kuhusu mkataba wa maegesho katikati ya jiji kupitia Kampuni ya National Parking System (NPS), alisema kamati hiyo pia imebaini kuwa Halmashauri ya Jiji imeiongezea mkataba wa miezi 10 kampuni hiyo kinyume cha taratibu wakati mkataba wake ulikuwa umeshamalizika.

Alisema mara baada ya mkataba huo kumalizika Agosti mwaka jana kampuni hiyo iliandikiwa barua ya kuongezewa mkataba wa miezi sita na baadaye miezi minne kwa madai kuwa mchakato wa kutafuta mzabuni bado haujakamilika.

“Kiutaratibu mheshimiwa Rais, mkataba unapoisha lazima ufanyike mchakato wa kutafuta mzabuni mpya na hata mwekezaji aliyepo anaruhusiwa kushiriki kuomba tena, lakini kilichofanyika ni kinyume kabisa, wakati tunajua kwa sasa eneo la mapato ya maegesho ni kubwa na maeneo mengi yameongezeka kuna nini hapa? Alihoji.

Alisema endapo viongozi hawatokuwa waaminifu katika maeneo mbalimbali yanayohusu fedha, kuna uwezekano mkubwa wa fedha za wananchi kupotea .

“Naomba Takukuru waendelee na uchunguzi wa suala hili ili waliohusika na haya wachukuliwe hatua,” alisisitiza Makonda.

 

Jumapili, Makonda alitoa ripoti ya kamati hiyo ndogo aliyoiunda na kutangaza wazi kuwasilisha majina ya Kabwe na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji, Sarah Yohana kwa mamlaka za kinidhamu ili wachukuliwe hatua kutokana na yaliyobainishwa kwenye mikataba hiyo.

Aidha aliweka wazi kuwa kutokana na madudu hayo yaliyobainishwa na kamati hiyo, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, hataki kufanya kazi tena na Kabwe pamoja Yohana.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By