Habarika | HALI YA GEORGE BUSH YATENGEMAA HUKU AKITARAJIWA KUHUDHURIA UAPISHWAJI WA DONALD TRUMP
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

HALI YA GEORGE BUSH YATENGEMAA HUKU AKITARAJIWA KUHUDHURIA UAPISHWAJI WA DONALD TRUMP

Vyombo vya habari nchini Marekani vimesema kuwa aliyekuwa rais wa taifa hilo George Bush anapata matibabu katika hispitali moja ya Houston katika jimbo la texas.

Maelezo kuhusu hali yake hayajatolewa ,lakini mkuu wa wafanyikazi wake amenukuliwa akisema kuwa bw Bush aliye na umri wa miaka 92 yuko katika hali nzuri na kwamba huenda akatolewa na kwenda nyumbani katika siku chache zijazo.

Bush kama marais wengine wa zamani anatarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Donald Trump katika sherehe itakayofanyika siku ya Ijumaa.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/hali-ya-george-bush-yatengemaa-huku-akitarajiwa-kuhudhuria-uapishwaji-wa-donald-trump/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By