Habarika | FLOYD MAYWEATHER AGOMA KURUDI ULINGONI
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

FLOYD MAYWEATHER AGOMA KURUDI ULINGONI

Mpiganaji masumbwi aliyestaafu katika tasnia hiyo ya ngumi za kulipwa, Mmarekani Floyd Mayweather amesema amepewa ofa ya pesa za kutosha kwa jili ya kurudi ulingoni.

Licha ya kumwagiwa pesa hizo zenye tarakimu tisa ambacho ni kiasi kikubwa cha pesa, lakini Mmarekani huyo ambaye alistaafu mwezi Septemba mwaka jana baada ya kushinda michezo 49 mfululizo ameweka wazi kwamba hayupo tayari kurudi ulingoni.

“Kwa sasa nishastaafu na kama ikitokea nikarudi basi haitakuwa kwa sababu ya pesa japokuwa itabidi nilipwe na ndio maana jina langu ni Floys “Money” Mayweather”, alisema nyota huyo mwenye miaka 38

Pambano la mwisho la bingwa huyo wa dunia katika uzito wa aina tano tofauti lilikuwa dhidi ya Andre Berto Septemba mwaka jana na akaibuka na ushindi ikiwa ni miezi mitatu tu baada ya kumtwanga mfilipo Manny Pacquiao katika pambano la karne lililopigwa kwenye dimba la MGM Grand Garden Arena huko Las vegas, Nevada.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By