Habarika | DUBAI YAUNDA WIZARA YA FURAHA NA UVUMILIVU
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

DUBAI YAUNDA WIZARA YA FURAHA NA UVUMILIVU

Waziri mkuu wa falme za kiarabu (UAE), Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, ametangazwa kuundwa kwa wizara mpya ya Furaha na Uvumilivu.

Wizara hiyo mpya imeundwa katika mabadiliko yaliyotekelezwa na utawala wa kiongozi wa UAE. Sheick Maktoum, ambaye ni kiongozi wa Dubai alisema Wizara hiyo mpya ya furaha ina lengo la kuhamasisha umma kutosheka na kile walichonacho. Wizara nyingine iliyoundwa ni wizara ya kuvumiliana.

Pia Sheick Maktoum, aliagiza kuunganishwa kwa baadhi ya wizara pamoja na kutoa zabuni kwa kampuni kuendesha asilimia kubwa ya shughuli za serikali. Kiongozi huyo alisema, haitaji wizara nyingi, bali kupata viongozi wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao.

Sheick Maktoum aliyasema hayo kwenye kongamano la dunia linalojadili miundo ya utawala na serikali mjini Dubai. “Tunachotaka ni serikali ndogo itakayokidhi matakwa ya vijana na umma kwa ujumla”, alisisitiza. Aliongeza kuwa, wizara ya uvumilivu itakuwa na lengo la kujenga umuhimu wa jamii kuvumilia katika miliki za mali walizonazo.

Pia sheick huyo, aliunda baraza maalum la vijana litakalokuwa likiishauri serikali ambapo baraza hilo litaongozwa na waziri mwanamke mwenye umri wa miaka 22.

CHANZO: UHURU

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/dubai-yaunda-wizara-ya-furaha-na-uvumilivu/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By