Habarika | DAWASCO KUPIGWA TAFU YA SH BILIONI 325.5 KUTOKA BENKI YA DUNIA ILI KUTOA HUDUMA BORA
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

DAWASCO KUPIGWA TAFU YA SH BILIONI 325.5 KUTOKA BENKI YA DUNIA ILI KUTOA HUDUMA BORA

Benki ya Dunia (WB) imeahidi kutoa kiasi cha Sh bilioni 325.5 kwa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya maji safi na maji taka katika maeneo mbalimbali yanayohudumiwa na shirika hilo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha sekta ya maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, hasa katika maeneo ambayo Dawasco inatoa huduma Dar es Salaam na miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bella Bird alisema hayo wakati wa kikao cha pamoja baina yake, Waziri wa Maji, Gerson Lwenge na viongozi wa Dawasco.

Kikao hicho kililenga kujadili uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.

Bird alionesha kuridhishwa na juhudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya maji safi, pamoja na kupambana na kiwango cha maji kinachopotea bila sababu ya msingi.

Alisema Benki ya Dunia imetenga fedha hizo kwa lengo la kuboresha miundombinu ya maji safi na maji taka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” iliyolenga kuwapunguzia akinamama wengi tatizo la maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa waathirika wakuu wa tatizo hilo.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na benki hiyo kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya maji.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/dawasco-kupigwa-tafu-ya-sh-bilioni-325-kutoka-benki-ya-dunia/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By