Habarika | CUF: TUTAUNGWA MKONO NA WAZANZIBARI KUTAFUTA HAKI KWA NJIA YOYOTE
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

CUF: TUTAUNGWA MKONO NA WAZANZIBARI KUTAFUTA HAKI KWA NJIA YOYOTE

Chama cha Wananchi CUF kimesisitiza kuwa kitaendelea na juhudi za kutafuta haki yake kwa njia yoyote na kina imani kuwa kitaugwa mkono na wananchi wa Zanzibar na kwa kuanzia wametangaza kutoitambua Serikali itakayoundwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein

Katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad aliwataka wananchi na wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho alisema CUF ipo katika juhudi za kutafuta haki wanayodai iliyotokana na kushinda katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ambao ulifutwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ambapo Maalim Seif alisema hayupo tayari kukaa meza moja na Dk Shein kwa ajili ya kutafuta suluhu ya Zanzibar

“Sipo tayari kukutana na Shein Ikulu kwa ajili ya mazungumzo ya kuleta amani na utulivi Zanzibar….nitakutana na yeye kama nani kwa sababu sisi CUF hatutambui ushindi wa Shein katika uchaguzi wa marudio pamoja na serikali yake”, alisema Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika serikali ya Umoja wa Kitaifa

Aidha, Baraza Kuu la CUF limepitisha maadhimio ya kuunga mkono uamuzi wa Marekani kuinyima Tanzania msaada kupitia Shirika la MCC hivi karibuni

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By