Habarika | Burudani
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

Burudani

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema wimbo wa Sizonje ulioimbwa na msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto ulitabiri utendaji kazi wa rais John Magufuli.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa Video ya wimbo huo jijini Dar es salaam, Nape alisema wimbo huo wa Mpoto unaonyesha njia ya Magufuli anavyotakiwa kufanya katika uongozi wake.

Alisema wimbo wa Sizonje umeimbwa kwa umaridadi mkubwa na umetungwa kwa maneno yenye maana na tija kubwa kwa viongozi, Katika uzinduzi huo ambao uliambatana na kuwapa tuzo wasanii waliofanya vizuri kwenye mtihani wa kidato cha nne hususani somo la Kiswahili, pia Nape ameahidi kumsaidia mwanafunzi aliyekuwa wa mwisho kitaifa katika mtihani huo hadi ahakikishe ndoto zake zinatimia licha ya kufeli.

Kwa upande wake Mpoto alisema ameamua kufanya tukio hilo la kauli mbiu ya kufeli shule sio kufeli maisha ili kila mwanafunzi ajue kuwa bado ana nafasi ya kutengeneza maisha yake.

Meya wa zamani wa jiji la New York nchini Marekani, Bwana Rudy Giuliani amechukizwa na kitendo cha mwanamuziki Beyonce Knowles kuonyesha ishara ya kisiasa ya “black power” wakati akitumbuiza kwenye fainali za 50 za mchezo maarufu wa American Football wakati wa muda wa mapumziko kwenye dimba la Levi’s huko jijini California.

Meya huyo amesema kwamba Beyonce hakutakiwa kufanya vile kwani pale ni sehemu mahususi kwa ajili ya michezo na sio Hollywood hivyo hakutakiwa kuonyesha ishara ile ya “Black Power” kwani ila lengo la kuwakashifu maofisa wa polisi ambao ni watu wanaowalinda wao na mali zao.

Ishara hiyo ya Black Power ilitumika mwaka 1968 na wanariadha wa Marekani Tommie Smith na John Carlos wakati wa sherehe za ugawaji tuzo katika michuano ya Olimpiki jijini Mexico City ikiwa ni ishara ya kudai usawa na  kupinga unyanyasaji wa watu weusi nchini Marekani ambao ulikuwa ukifanywa na maofisa wa polisi kwa amri ya serikali ya watu weupe.

” Tunachotakiwa kuwa tunafanya katika jamii zenye mchanganyiko wa watu weusi na weupe na jamii zote kwa ujumla ni kuwaheshimu polisi kwasababu wanajitolea maisha yao kwa ajili yetu, sijapendezwa na kitendo cha Beyonce kutumia shoo yake  kuonyesha ishara ambazo zinaleta uchochezi hasahasa ikiwa ni kejeli kwa jeshi la polisi”. Alisema Rudy Giulian.

beyonce3

Katika shoo hiyo ambayo Beyonce alitumbuiza kwa wimbo wake maarufu wa “Formation” ambao Giulian aliuita ni wimbo wenye uchochezi wa kisiasa ndani yake, wacheza shoo wa Beyonce walivaa nguo nyeusi ambazo ni ishara ya wanaharakati weusi “black panthers” ambacho kilikuwa ni chama cha watu weusi kilichoundwa kupigania haki za watu hao dhidi ya unyanyasaji wa watu weupe nchini humo miaka 50 iliyopita na kumfanya meya huyo kumkosoa Beyonce hususani pale yeye na kundi lake waliponyanyua kiganja juu kilichokunjwa kwa ishara ya ngumi ambacho kilitumika miaka ya nyuma kuashiria umoja wa watu weusi yaani “black power”.

 

Mwanamuziki nguli wa HipHop wa nchini Marekan Clifford Joseph Harris, Jr., maarufu kama T.I na mkewe Tameka Pope maarufu kama Tiny wanatarajia kupata mtoto wao wa pili hivi karibuni.

Endapo watafanikiwa kupata mtoto huyo basi T.I atakuwa na jumla ya watoto sita, lakini kwa Tiny atakuwa na watoto watatu.

“Ni furaha kubwa kuona familia yetu inaongezeka, tunatarajia kupata mtoto hivi karibuni, hii ni zawadi kutoka kwa Mungu,” alisema Tiny.

T.I ni miongoni mwa wasanii ambao wana watoto wengi nchini Marekani kama vile DMX ambaye ana watoto 12.

Kupitia mtandao wa Instagram, Tiny aliweka picha yake na kudai kwamba wanashukuru Mungu kwa kuwapa zawadi mpya.

“Tuna furaha kubwa sana kwa zawadi ambayo tunaitarajia hivi karibuni ya mtoto ambaye yuko njiani kwa sasa,” aliandika Tiny.