Habarika | BUNGE LASIMAMISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI MIPYA YA NSSF
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

BUNGE LASIMAMISHA UTEKELEZAJI WA MIRADI MIPYA YA NSSF

Bunge limesimamisha utekelezaji wa miradi yote mipya ya shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mpaka hapo kamati na Wizara itakapopitia taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za serikali (CAG), sambamba na kuitisha taarifa za utekelezaji wa miradi yote iliyofanywa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Aidha, imeagiza ukaguzi wa kina wa ujenzi wa jengo jipya la Ofisi za Makamu wa Rais kwa kuangalia usalama wa jengo, hesabu zilizotumika kama zinaendana na thamani ya jengo na kama washauri walitoa ushauri wao ipasavyo.

Akizungumza katika kuhitimisha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya serikali iliyofanywa na Kamati ya Katiba na Sheria, Mwenyekiti wa kamati ya katiba na sheria, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa alisema NSSF ilitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ikiwa haijitoshelezi kwa kutoonesha gharama zilizotumika mpaka sasa, bajeti iliyopangwa kutumika kwa kiasi kilichosalia ili kubaini kama fedha zilizotumika zinalingana na thamani ya ujenzi wenyewe

Akizungumzia taarifa za utekelezaji wa miradi iliyofanywa na mifuko yote ya hifadhi ya jamii, Mchegerwa alisema kamati yake inataka kupitia taarifa zote za utekelezaji wa miradi sambamba na kupitia sera ya uwekezaji ili kuangalia kama yamefuata utaratibu na hakuna upotoshaji

“Kuna kuna madeni makubwa ambayo mifuko hiyo inadai kwa wapangaji wao. Pia tunaangalia sera ya uwekezaji ili kujiridhisha kama ushauri wa kitaalamu uliotolewa unakidhi matakwa ya ujenzi unaoendelea”.

 

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/bunge-lasimamisha-utekelezaji-wa-miradi-mipya-ya-nssf/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By