Habarika | Biashara
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

Biashara

Kampuni ya matangazo ya kidigitali ya Smartcodes imezindua rasmi mtandao ujulikanao kama “Kwanza” ambalo ni jukwaa mahsusi kwa ajili ya kujumuisha matangazo yote ya kidigitali ndani ya mtandao mmoja Tanzania.

Jukwaa hilo la kitaalamu la ‘Kwanza’ ambalo ni la kwanza kwa Tanzania litawezesha bidhaa na watangazaji wa bidhaa hizo kuwafikia mamilioni ya watumiaji kupitia simu zao za mikononi, tovuti na kifaa chochote kinachotumia mtandao (internet)

kwanza2

 Akiuzungumzia mtandao huo, Edwin Bruno ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Smart Codes amesema kuwa mtandao huo una lengo la kutatua matatizo ya kuwafikia watumiaji walengwa wa bidhaa kupitia simu zao za mikononi kitu ambacho kimekuwa ni changamoto kubwa katika taaluma ya masoko kwa sasa

“Kwa nchi kama ya Tanzania yenye watumiaji wa mtandao zaidi ya milioni 17.26, changamoto iliyozoeleka kwa wanataaluma wa masoko limekuwa ni kuwaelewa na kuwatambua watumiaji kupitia vifaa vyao, jinsi ya kuwalenga na mwisho upimaji sahihi wa matangazo yaliyonunuliwa”, Alisema Edwin Bruno, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Smart Codes.

“Kwanza inafanya bidhaa kuwalenga watumiaji wake kulingana na eneo husika kwa kutumia kifaa tu au mfumo wa uendeshaji kwa muda muafaka, siku ndani ya wiki au mwezi. Kwa mfano, kama biashara yako ipo Dar, kwanini upoteze matangazo yako ya thamani kwa watumiaji wa Mtwara? Alifafanua Edwin Bruno

Naye Herman Mkamba ambaye ni Mnunuzi wa Matangazo ya Mitandaoni wa Kampuni hiyo ya Smart Codes ameongeza kuwa app hiyo ya Kwanza itakuwa ikitoa taarifa sahihi kwa kampeni za matangazo, kiasi kilichotumika na matangazo yanayofanya vyema.

“Taarifa zote zitakuwa zikipatikana kwenye dashibodi ya mtangazaji mwenyewe na kwenye app ya Android ya Kwanza. Ukiwa na app hii utapata muhtasari na takwimu za kina ikiwa ni pamoja na kutengeneza na kusimamisha kampeni, kuweza kupata rekodi ya matumizi na usawa, kuona wapi na matangazo gani yanafanya vizuri ambapo hayo yote utakuwa ukiyapata kwa kutumia ncha za vidole vyako, popote na muda wowote”, alimalizia Herman Mkamba.

“Tanzania inatakiwa kujifunza kutoka Bara la Asia katika uanzishwaji wa viwanda. nchi za Korea Kusini, taiwan, Hong Kong na Singapore zilifanikiwa kuingia kwenye uchumi wa viwanda baada ya kuangalia kile walichozalisha na sio kinachozalishwa nje ya nchi yao..”

Mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka China, Justin Lin amesema iwapo Tanzania inataka kuelekea kwenye uchumi wa viwanda, ni lazima itumie mbinu zilizotumiwa na nchi za Asia kwa kuanzisha viwanda vidogo vyenye kuajiri watu wengi ambayo malighafi zake zinapatikana ndani ya nchi.

Akizungumza kwenye kongamano la kujadili mbinu za kuufikia uchumi wa viwanda lililoandaliwa na Asasi ya utafiti ya Uchumi na kupunguza Umasikini (Repoa), Lin alisema, nchi za Asia miaka 30 iliyopita zilikuwa masikini, lakini ziligeukia uchumiwa viwanda kwa kuangalia walichonacho na wanachozalisha na kuamua kukiongezea thamani.

“Tanzania inatakiwa kujifunza kutoka Bara la Asia katika uanzishwaji wa viwanda. nchi za Korea Kusini, taiwan, Hong Kong na Singapore zilifanikiwa kuingia kwenye uchumi wa viwanda baada ya kuangalia kile walichozalisha na sio kinachozalishwa nje ya nchi yao..”

“Afrika na Tanzania ziangalie zinazalisha nini kwa sasa, hicho ndicho wakiwekee mikakati ya kuanzisha viwanda vitakavyosaidia kuongeza thamani mazao na bidhaa nyingine zilizopo ndani ya nachi zao ili ziweze kupata soko zuri”, alisema mtaalamu huyo wa uchumi.

Kampuni inayoongoza katika teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) duniani ya HUAWEI imetangaza uteuzi wa mwanasoka bora wa dunia na mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona Lionel Messi kuwa balozi wake ambapo shirikiano huo kati ya Messi na Huawei, unaonyesha jinsi gani kampuni hiyo nguli duniani ilivyojipanga kuunganisha mwanasoka bora duniani, nabidhaa bora duniani.

methi 3

Akizungumzia uteuzi huo, mkurugenzi mtendaji wa Huawei kanda ya Afrika Peter Hu alisema “Tuna furaha kutangaza ushirikiano na mwanasoka mwenye kipaji cha kipekee anayewatia moyo mamilioni ya watu duniani kufata ndoto zao, kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo na kuwa na mafanikio kila siku. Messi anaamini katika ubora wa bidhaa na huduma zaHuawei, kama sisi, naye daima anatafuta fursa za kufikia ubora zaidi.”

Akizungumzia ushirikiano huo, Lionel Messi alisema “Ni lazima upambane ili kufikia ndoto zako, ni lazima ujitoe haswaa, daima ukitazama mbele ili kufikia ubora unaoutaka. Siku unayodhani kuwa hakuna mabadiliko zaidi, ni mwanzo wa kuanza upya kufikia mafanikio mengine”

Akizungumzia uwekezaji wa Huawei barani Afrika, Hu alisema “Dhamira ya Huawei kwa bara la Afrika inaweza kuonekana kwa kutazama kiasi gani Huawei zinabadili maisha ya waafrika. Katika ukanda wa Africa kusini na mashariki mwaAfrika, Huawei inashikilia namba mbili (2) kwa usambazaji wa simu janja (Smartphones). Kwa upande mwingine, tafiti za masoko zinaonyesha kuwa, Huawei inashikilia karibu asilimia 15% ya simu janja zote katika ukanda huo. Pia tunaendelea kuleta na kusambaza zaidi simu za kiwango cha juu, kwa mfano Huawei P8 Lite ilishinda tuzo hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini.”

methi2

“Lionel Messi atasaidia watu wengi zaidi, hasa waafrika kuzingatia, kuwa na subirá na uvumilivu na baadaye kufanikiwa kuunganishwa na UKUU.  Kwa kuunganisha ukuu, sisi kama Huawei, tunaonyesha shauku zetu kwa wateja wetu ” alihitimisha, Hu.

 

Watanzania wamepewa mwito kujenga tabia ya kujiwekea akiba benki kwa ajili ya manufaa yao na taifa.

Meneja wa fedha na utawala wa Bodi ya Bima na Amana (DIB) iliyo chini ya benki kuu ya Tanzania (BoT), Richard Malisa alitoa mwito huo juzi wakati akitoa mada kwenye semina ya kuwajengea wanahabari uwezo wa kuandika na kusambaza habari za sekta ya biashara, uchumi na fedha.

“Pesa zinapowekwa benki hutumika kuchangia kuinua na kuimarisha usalama wa akiba ya mtu binafsi na kwa upande wa nchi inatumika katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuinua sekta ya elimu, afya, maji, ujenzi wa barabara na kilimo” alisema Malisa

Alisema, taasisi au mtu binafsi anapoweka fedha benki, anauwa amejiwekea amana kubwa na muhimu kwa kuwa tabia hiyo ya uwekaji fedha ina tija na inaongeza usalama.

Alishauri Watanzania kuwa makini na uchukuaji mikoo kuepuka kufuata mkumbo au kushinikizwa

Benki ya Barclays Tanzania (BBT) imewahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma za kibenki hapa nchini, pamoja na kuwapo kusudio la kampuni mama la kupunguza hisa kwa Barclays Afrika.

Barclays London yenye hisa ya 62.3 katika kampuni yake tanzu ya Barclays Afrika inakusudia kupunguza hisa zake ndani ya miaka miwili au mitatu ijayo ili kwenda sambamba na sera za fedha za Marekani na Uingereza ambazo zinataka benki hiyo kupunguza hisa zake Afrika.

Mkurugenzi mtendaji wa Barclays Tanzania, Kihara Maina, alisema shughuli za Barclays Afrika sambamba na Tanzania zitaendelea kuwapo sambamba na kufanya mikakati ya kufanya mabadiliko.

“Tutaendelea kutoa huduma zetu katika soko la Tanzania, hatutakuwa na mabadiliko yoyote, Mfumo wa hisa utabadilika lakini mikakati yetu haitabadilika”, alisema Maina.

Maina aliongeza: “ Hakuna kitakachobadilika na niwahakikishie wateja wetu kuwa fedha zao ziko salama. Wafanyakazi nao wako salama na watawahudumia wateja wetu. Benki iko vizuri kwa kuwa na mtaji ambao utaifanya kuwa benki bora nchini.

Barclays inamilikiwa na Barclays Afrika kwa asilimia 100 na ina wateja 80,000 na wafanyakazi 500. Awali akizungumza na waandishi wa habari moja kwa moja kutokea Afrika Kusini, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Maria Ramos alisema mwaka jana kampuni yake ilipata faida kwa asilimia 8 ambazo ni randi bilioni 29.5 wakati faida iliyokokotolewa ni asilimia 17 ambayo sawa na randi bilioni 2.3

-HABARI LEO

Wizara ya Fedha na Mipango kupitia mamlaka ya Masoko, Mitaji na Dhamana (CMSA) mkoani Lindi itasimamia mauzo ya korosho na ufuta katika mfumo wa stakabadhi kwa msimu wa mwaka huu.

Meneja wa uhusiano wa CMSA, Charles Shirima, alisema hali hiyo itaweza kuondoa migongano baina ya wakulima, vyama vya msingi vya ushirika na wanunuzi, wakati wa mauzo ya mazao hayo na malipo.

Shirima alisema hayo wakati alipokuwa akiitambulisha taasisi hiyo ya serikali kwa viongozi wa ngazi ya ofisi ya mkuu wa mkoa, wilaya, makundi ya wakulima, kamati ya muda ya chama Kikuu cha Ushirika Lindi mwambao juu ya kusimamia kimauzo mazao hayo katika msimu wa mwaka huu.

Shirima alisema uanzishwaji wa soko la bidhaa utaweza kuleta mawasiliano na sekta za fedha, miundombinu na mfumo wa stakabadhi kwa baadhi ya mazao.

Alisema kwamba maendeleo hayo yanatoa fursa za kuboresha mfumo wa masoko nchini ili kuleta mfumo wenye ushindani na ulio wazi na ambao utaweza kumfanya mkulima aweze kunufaika na juhudi zake.

Kwa mujibu wa Shirima, kuondoa migongano kutaweza kuleta chachu kwa wakulima kuweza kuzalisha kwa wingi kutokana na kuwepo kwa masoko mbalimbali ya mazao hayo.

Naye mchambuzi wa fedha wa mamlaka hiyo, Witness Gowelle alisema mamlaka hiyo isimamie kwa mara ya kwanza kwa mazao ghafi na kutafutiwa masoko.

-HABARI LEO

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame  Mbarawa amewataka watendaji wa Shirika la Posta Tanzania na   Kampuni ya simu ya (TTCL) kufanya kazi kwa weledi na mtazamo  wa kibiashara  ili kuyaongezea mapato mashirika hayo na hivyo  kuendana na  mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanaoyotokea nchini.

Akizungumza na wafanyakazi wa TTCL na POSTA mkoani Mwanza Prof. Mbarawa amesema kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano duniani, biashara ya simu na posta hivi sasa zina ushindani mkubwa unaohitaji mtazamo mpana wa kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko.

“Serikali inajitahidi kuisaidia TTCL na POSTA hivyo wekezeni vizuri kwenye data na uharaka wa utoaji huduma ili muweze kushindana kwenye soko na kukuza uchumi wa taasisi hizi muhimu kwa usitawi wa nchi”, amesema Prof Mbarawa.

Prof. Mbarawa amezitaka menejimenti za POSTA na TTCL kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu ili malengo na mikakati ya taasisi hizo yafahamike kwa wafanyakazi wote na kuwezesha kujipima kama wanafikia malengo yaliyokusudiwa.

“Hakikisheni wafanyakazi wote wanaelewa malengo na mikakati ya tasisi zenu ili kazi ya kuyatekeleza ifanywe kwa umoja na ushirikiano”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

CHANZO: TUAMBIE

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imeshusha bei ya mafuta ya aina ya dizeli kwa sh 1,600 kwa mkoa wa Dar es Salaam kutoka sh. 1,747

Punguzo hilo la bei ni sawa na sh. 147 kwa lita huku petroli ikishuka kwa sh. 55 na kufanya mafuta hayo kuuzwa sh, 1,842 kutoka 1,899 tangu mwezi uliopita.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi alisema kushuka kwa bei hizo zinatokana na kuendelea kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji nchini.

“Hakukuwa na mafuta ya taa yaliyoingiza nchini Januari 2016, hivyo mwezi Februari bei itaendela kama ilivyokuwa kwa mwezi Januari, ambayo ni sh. 1,699 kwa lita kwa soko la Dar re Salaam,” alisema

Alisema kushuka kwa namna hii kulitokea Machi mwaka jana, ambapo lita moja ya mafuta ya dizeli ilishuka hadi kufikia sh. 145 na kufanya kuwa sh. 1,563

“Aidha ni muhimu kuzingatia kuwa kushuka kwa bei za mafuta masafi (siyo ghafi) katika soko la dunia huchangia takribani asilimia 46 mpaka 49 ya bei katika soko la ndani kwa bei za January mwaka huu, hivyo kushuka huko hakuwezi kuwa na uwiano asilimia 100 kushuka kwa bei katika soko la ndani,” alisema

Aliongeza kuwa EWURA imevikumbusha vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani,” alisema

Ngamlagosi alisema ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika, pia EWURA inawashawishi wanunuzi kuhakikisha wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta na bei husika.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, ndugu William Lukuvi (mb) ameliagiza Shirika la Nyumbala Taifa NHC kujenga nyumba za gharama nafuu utakaokuwa na ukweli wa unafuu huo.

Hayo yameelezwa alipotembelea ofisi za shirika hilo mkoani Mbeya ambazo pia huhudumia mkoa wa Njombe. Lukuvi alisema

“Acheni kuilalamikia serikali kwa kuchukua fedha za ongezeko la thamani (VAT) kwamba ndio inayoongeza gharama za ujenzi.”

Lukuvi alilitaka shirika hilo kufanya utafiti wa kina juu ya namna gani linaweza kujenga nyumba za gharama nafuu kiukwelikweli ambazo zitaweza kujengwa mijini na kwenye miji midogo midogo vijijini.