Habarika | BENKI YA BARCLAYS KUENDELEA KUTOA HUDUMA NCHINI
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

BENKI YA BARCLAYS KUENDELEA KUTOA HUDUMA NCHINI

Benki ya Barclays Tanzania (BBT) imewahakikishia wateja wake kuwa itaendelea kutoa huduma za kibenki hapa nchini, pamoja na kuwapo kusudio la kampuni mama la kupunguza hisa kwa Barclays Afrika.

Barclays London yenye hisa ya 62.3 katika kampuni yake tanzu ya Barclays Afrika inakusudia kupunguza hisa zake ndani ya miaka miwili au mitatu ijayo ili kwenda sambamba na sera za fedha za Marekani na Uingereza ambazo zinataka benki hiyo kupunguza hisa zake Afrika.

Mkurugenzi mtendaji wa Barclays Tanzania, Kihara Maina, alisema shughuli za Barclays Afrika sambamba na Tanzania zitaendelea kuwapo sambamba na kufanya mikakati ya kufanya mabadiliko.

“Tutaendelea kutoa huduma zetu katika soko la Tanzania, hatutakuwa na mabadiliko yoyote, Mfumo wa hisa utabadilika lakini mikakati yetu haitabadilika”, alisema Maina.

Maina aliongeza: “ Hakuna kitakachobadilika na niwahakikishie wateja wetu kuwa fedha zao ziko salama. Wafanyakazi nao wako salama na watawahudumia wateja wetu. Benki iko vizuri kwa kuwa na mtaji ambao utaifanya kuwa benki bora nchini.

Barclays inamilikiwa na Barclays Afrika kwa asilimia 100 na ina wateja 80,000 na wafanyakazi 500. Awali akizungumza na waandishi wa habari moja kwa moja kutokea Afrika Kusini, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Barclays Afrika, Maria Ramos alisema mwaka jana kampuni yake ilipata faida kwa asilimia 8 ambazo ni randi bilioni 29.5 wakati faida iliyokokotolewa ni asilimia 17 ambayo sawa na randi bilioni 2.3

-HABARI LEO

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By