Habarika | BEI YA MAFUTA YASHUKA TENA
layout-wrap boxed
Friday, April 27, 2018

BEI YA MAFUTA YASHUKA TENA

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imeshusha bei ya mafuta ya aina ya dizeli kwa sh 1,600 kwa mkoa wa Dar es Salaam kutoka sh. 1,747

Punguzo hilo la bei ni sawa na sh. 147 kwa lita huku petroli ikishuka kwa sh. 55 na kufanya mafuta hayo kuuzwa sh, 1,842 kutoka 1,899 tangu mwezi uliopita.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi alisema kushuka kwa bei hizo zinatokana na kuendelea kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji nchini.

“Hakukuwa na mafuta ya taa yaliyoingiza nchini Januari 2016, hivyo mwezi Februari bei itaendela kama ilivyokuwa kwa mwezi Januari, ambayo ni sh. 1,699 kwa lita kwa soko la Dar re Salaam,” alisema

Alisema kushuka kwa namna hii kulitokea Machi mwaka jana, ambapo lita moja ya mafuta ya dizeli ilishuka hadi kufikia sh. 145 na kufanya kuwa sh. 1,563

“Aidha ni muhimu kuzingatia kuwa kushuka kwa bei za mafuta masafi (siyo ghafi) katika soko la dunia huchangia takribani asilimia 46 mpaka 49 ya bei katika soko la ndani kwa bei za January mwaka huu, hivyo kushuka huko hakuwezi kuwa na uwiano asilimia 100 kushuka kwa bei katika soko la ndani,” alisema

Aliongeza kuwa EWURA imevikumbusha vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani,” alisema

Ngamlagosi alisema ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika, pia EWURA inawashawishi wanunuzi kuhakikisha wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta na bei husika.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

Sambaza Makala hii: Share on Facebook2Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By