Habarika | BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LAAPISHWA ZANZIBAR
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI LAAPISHWA ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein amewaapisha  Mawaziri na Manaibu mawaziri wa Wizara 13 za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri wasiokuwa na Wizara Maalumu ambao pia ni wajumbe wa Baraza la Mapinduzi.

Mawaziri hao waliapishwa jana katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama na serikali pamoja na wananchi kadhaa.

Baraza hilo la Mawaziri lililotangazwa juzi, lina sura mpya nane likijumuisha wajumbe kutoka katika vyama vya siasa vya upinzani, wanasiasa mashuhuri visiwani humo, huku manaibu waziri saba wote wakiwa wageni katika nafasi hiyo.

Wapinzani walioteuliwa ni Hamad Rashid Mohammed ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha ADC aliyeapishwa kuwa Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Wengine ni Said Soud Said kutoka AFP na Juma Ali Khatibu kutoka TADEA ambao wanakuwa mawaziri wasiokuwa na wizara maalumu

Miongoni wa waliohudhuria hafla hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, Spika wa baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid.

Wengine ni mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Said Hassan Said, Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Shehe Khamis Haji na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdala Mwinyi Khamis; Meya wa Manispaa ya mji wa Zanzibar Khatib Abrahaman Khatib pamoja na viongozi wa vikosi vya ulinzi.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/baraza-jipya-la-mawaziri-laapishwa-zanzibar/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By