Habarika | KATIKA KUBORESHA UHUSIANO WA KIBIASHARA; BALOZI WA BRAZIL AIHIMIZA TANZANIA KUNUNUA NDEGE NCHINI MWAO
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

KATIKA KUBORESHA UHUSIANO WA KIBIASHARA; BALOZI WA BRAZIL AIHIMIZA TANZANIA KUNUNUA NDEGE NCHINI MWAO

Mabalozi wa Brazil na Kenya nchini wameipongeza serikali ya Tanzania kwa mipango na mikakati yake ya kulifufua shirika la ndege nchi ATCL kwa kununua ndege mpya hatua ambayo itasaidia kukuza shughuli za utalii na pato la Taifa.

Mabalozi hao wametoa pongezi hizo mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa rais, Bi Samia Suluhu Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake balozi wa Brazil Carlos Alphonce, amesema kutokana na nchi hiyo kuwa ni nchi yenye viwanda vya kutengeneza ndege duniani amesema serikali ya Tanzania ina nafasi nzuri ya kununua ndege nchini humo.

Naye Makamu wa rais amewakaribisha wawekezaji wa Brazil kuja nchi kutangaza bidhaa wanazo zitengeneza hasa ndege hatua ya kuimarisha mahusiano ya biashara kati ya nchi hizo. Na kwa upande wake balozi wa Kenya nchini, Chilau Makwere, amesisitiza kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Kenya hasa katika uimarishaji wa biashara na uwekezaji.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By