Habarika | ASKARI WA JWTZ WANAONYANG'ANYA WAVUVI SAMAKI KUCHUKULIWA HATUA
layout-wrap boxed
Sunday, February 25, 2018

ASKARI WA JWTZ WANAONYANG’ANYA WAVUVI SAMAKI KUCHUKULIWA HATUA

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanadaiwa kuwanyanyasa wavuvi kwa kuwanyang’anya samaki wao, Bunge limeelezwa. Maeneo yaliyotajwa kukithiri kwa unyanyasaji huo ni Kigamboni na Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako wanajeshi hao wanatuhumiwa pia kuwanyang’anya leseni wavuvi hao wakidai hazitakiwi kwa ajili ya uvuvi huo.

Madai hayo yalitolewa na Mbunge wa Bumbwini, Muhammed Amour Muhammed (CUF) katika swali lake la msingi ambalo alitaka kufahamu mpango wa serikali wa kuondoa unyanyasaji huo unaofanywa na JWTZ dhidi ya wananchi wake.

Akijibu swali hilo la msingi, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alisema wizara yake haijawahi kupokea tuhuma yoyote inayohusu unyanyasaji unaofanywa na askari wa JWTZ kwa wavuvi nchini.

“Kama tuhuma hizi zina ushahidi ni bora zikafikishwa sehemu husika ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua zinazostahili,” alisema Dk Mwinyi. Dk Mwinyi alisema wanajeshi kama walivyo raia wote wanapaswa kuheshimu sheria za nchi na pale wanapokwenda kinyume huchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa sheria na kanuni za jeshi hilo.

Mbunge huyo katika swali lake la nyongeza alisema ana ushahidi wa watu walionyang’anywa samaki na askari hao wa JWTZ waliokuwa wakiwaambia leseni zao sio zinazotakiwa pamoja na kumhoji waziri huyo kama yupo tayari kufuatana naye akawaone waathirika hao.

Dk Mwinyi alitaka ushahidi huo ufikishwe sehemu husika ili uchunguzi ufanyike na kueleza kuwa yupo tayari kuongozana na mbunge huyo kwenda kuwaona wavuvi hao wanaodai kunyanyaswa na askari wa JWTZ. Kuhusu suala la leseni, alisema “leseni ipo chini ya Wizara ya Uvuvi (Kilimo na Mifugo), JWTZ si kazi yao kuangalia leseni isipokuwa ni kuangalia uvuvi haramu.”

Sambaza Makala hii: Share on Facebook0Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone


Warning: file_get_contents(http://graph.facebook.com/?ids=http://habarika.com/askari-wa-jwtz-wanaowanyanganya-wavuvi-samaki-kuchukuliwa-hatua/): failed to open stream: HTTP request failed! HTTP/1.1 403 Forbidden in /home/habarika/public_html/wp-content/themes/habarika/elements/element.php on line 80
0 comments

By