Habarika | ASKARI POLISI WATUPWA JELA MIAKA 20 KWA WIZI WA MENO YA TEMBO
layout-wrap boxed
Sunday, April 22, 2018

ASKARI POLISI WATUPWA JELA MIAKA 20 KWA WIZI WA MENO YA TEMBO

Watu nane wakiwemo waliokuwa askari polisi wawili wa kanda maalumu ya Polisi, Dar es Salaam wamehukumiwa miaka 160 jela huku mmoja akiachiwa huru baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na vipande 70 vya meno ya tembo.

Watu hao walipatikana na hatia hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Kibaha mkoani Kibaha ambapo hukumu hiyo imetolewa jana na hakimu wa mahakama hiyo Herieth Mwailolo.

Mbali ya kukutwa na hatia hiyo pia walibainika kuwa walikuwa wakijihusisha na kuendesha genge la uhalifu wa makosa ya uhujumu uchumi kwa watuhumiwa wawili ambao ni Koplo Senga Nyembi mwenye namba D 8656 na PC Issa Mtama mwenye namba G 553.

Watuhumiwa wengine ni Prosper Maleto, Seif Mdumuka, Amri Bakari, Said Mdumuka, Ramadhani Athuman na Musa Mohamed na dereva Hamidu Hamad ambaye aliachiwa huru baada ya mahakama kujiridhisha na utetezi aliouwasilisha mahakamani hapo kwani alisimamishwa na askari hao kuombwa msaada kupeleka watuhumiwa kituo cha polisi Kisarawe lakini walikamatwa kabla ya kufika kwenye kituo hicho.

Wahukumiwa hao walihukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja na kulipa faini ya Sh bilioni 8.5 kwa kosa la kwanza,kifungo cha miaka 15 kila mmoja kwa mtuhumiwa wa kwanza na wa pili ambapo adhabu zote zitakwenda kwa pamoja

Aidha mahakama imetaifisha gari lililobeba men ohayo ya tembo ambapo gari hilo ni lenye namba za usajili T359 ABK aina ya Tooyota Surf.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook4Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By