Habarika | AL SHABAB YAKANUSHA KUUAWA KWA WANAMGAMBO WAKE 150
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

AL SHABAB YAKANUSHA KUUAWA KWA WANAMGAMBO WAKE 150

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab nchini Somalia limethibitisha kwamba maeneo yake yalishambuliwa kwa mabomu na Marekani.

Hata hivyo, kundi hilo limesema taarifa kwamba zaidi ya wanamgambo 150 waliuawa kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa na ndege zisizo na rubani “zaimetiwa chumvi”.

Wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema wapiganaji 150 wa al-Shabab waliuawa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa Jumamosi katika kambi ya mazoezi ya wanamgambo hao.

“Marekani ilirusha mabomu katika eneo linalodhibitiwa na al-Shabab. Lakini walitia chumvi kwenye idadi ya waliofariki. Hatuwezi kuwaweka pamoja wapiganaji 100 kwa sababu za kiusalama. Tunajua kumejaa ndege angani,” msemaji wa kundi hilo Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia Reuters.

Hata hivyo hakusema ni wapiganaji wangapi wa kundi hilo waliuawa.

Sambaza Makala hii: Share on Facebook3Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By