Afisa mmoja wa polisi amefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe baada ya kushtakiwa kwa kumkashifuku Rais Robert Mugabe baada ya kudai kuwa Rais huyo mwenye umri wa miaka 92 ni mzee sana kuwa kiongozi.
Thomson Joseph Mloyi pia anadaiwa kumtukana mke wa Rais Mugabe, bibi Grace, kuwa ni kahaba kwa mujibu wa gazeti binafsi la nchini humo.
Bwana Mloyi aliachiliwa kwa dhamana ya dola 100 na anatarajiwa kufikishwa mahakamani tena tarehe 15 mwezi huu.
Mugabe ndiye kiongozi wa umri mkubwa zaidi duniani baada ya kutimiza umri wa miaka 92 mwezi uliopita.
0 comments