Habarika | WATU 52 WAKWAMA MGODINI AFRIKA KUSINI
layout-wrap boxed
Tuesday, May 22, 2018

WATU 52 WAKWAMA MGODINI AFRIKA KUSINI

Chombo cha habari cha News24 kinaripoti kuwa takriban wachimba mgodi 52 wamekwama ardhini ndani ya mgodi wa dhahabu mashariki mwa Afrika Kusini.

Daktari mmoja wa kutoa matibabu ya dharura nchini humo Jacques Ainslie alisema kuwa kisa hicho kilitokea mwendo wa saa mbili asubuhi ambapo  mojawapo ya shimo liliporomoka na kuwanasa wachimba mgodi 52 huku akiongeza kuwa mpaka kufikia sasa asilimia 70 ya wachimba mgodi hao ambao ni sawa na wafanyakazi 30 wameokolewa.

Hata hivyo bwana Ainsilie ameongeza kuwa wachimba mgodi waliojeruhiwa wamesafirishwa katika hospitali moja kwa matibabu wakati huohuo watu watatu bado hawajulikani waliko na bwana Anslie amesema anashuku huenda wamekwama katika chumba ambapo mporomoko huo ulianza.

CHANZO: BBC SWAHILI

Sambaza Makala hii: Share on Facebook1Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn0Share on Google+0Email this to someone

You may also like

0 comments

By